- Adamu Mwenziwe Hawa,Mwanamume Na Mkewe
- Adui Huletwa Na Kisasi
- Afadhali Ndoa Mbaya Kuliko Ujane Mwema
- Afuatanae Na Bwana,Bwana Naye
- Aibu Si Kitendo, Aibu Ni masimulizi
- Ajaye Haulizwi Nani, Mwache Afike
- Ajizi Nyumba Ya Njaa
- Akili Haba Na Madaraka Makubwa Msiba
- Akili Razini Ni Afya Mwilini
- Aakuitaye Kajaza Ukikawia Hupunguza
- Aliye Na Umbu, Hakosi Mwamu
- Angenda Juu Kiboko,Makazi Yake Majini
- Asiye Safari Husifu Upishi Wa Mama Yake Tu .
- Bahati Hutaka Ujasiri
- Bahati Teuzi Haiendi Kwa Kila Mtu
- Bei Ni Mghalaba
- Bidii Ya Mchwa Hujenga Nyumba Kwa Mate
- Bila Mapenzi Dunia Hatuiwezi
- Bora Adui Mwerevu Kuliko Rafiki Mjinga
- Bweta La Siri Ni Moyo
- Chakuota Si Chakuiba,Cha Mchongoma Kina Mwiba
- Cha Mjinga Huzama ,Cha Mwerevu Huelea
- Chakula Ni Wali Kiungo Ni Samli,Na Mke Ni Mwanamwali
- Chanda Na Pete ,Ulimi Na Mate Uta Na Upote
- Chandugu Hakiwi Chako Sharti Upewe
- Chawa Si Mzito Lakini Husumbua
- Chechema Utafika Uendako
- Chema Huta Kwa Na Mungu Na Watu
- Cheupe Dawa Cheusi Badili Hawa
- Chini Kwetu Juu Kwa Mungu
- Chini Ya Wadogo Juu Ya Wakubwa
- Chongo Kwa Mnyamwezi,Kwa Mswahili Rehema Ya Mungu
- Chuma Kipate Kingali Moto
- Chungu Huvunjika Magae ,Na Mtu Huharibika Asifae
- Dalili Ya Vita Matata
- Dhahabu Haina Maana Chini Ya Ardhi
- Dhihaka Ina Kweli Ndani Yake
- Dunia Mapito Haiachi Unyayo Wala Alama
- Elimu Bahari Haikaushiki
- Elimu Bahari Haiishi Kwa Kuchotwa
- Elimu Bila Adili Ni Ujahili
- Epukae Uovu Si Mpumbavu
- Fadhili Ya Nyuki Ni Moto
- Farasi Humuwawezi, Ndovu Mtawalishani?
- Furaha Ya Mchezoni Usiende Nayo Vitani
- Fuata Hekima Uwe Na Heshima
- Fundi Hawi Mwanafunzi,Mkulima Haagilizi
- Gharama Ya Dhambi Kubwa Kuliko Ya Dhawabu
- Gurudumu La Maisha Ni Tama
- Gurudumu Limefupisha Umbali
- Hadhi Huugua Lakini Haifi
- Hakuna Bamvua Lisilo Usubi
- Hana Bwando Mtu Wa Vishindo
- Hana Nafuu Mwenye Makuu
- Heri Kuliwa Na Samba Kuliko Kuliwa Na Fisi
- Hasira Haijui Manza
- Heri Jirani Kuliko Rafiki Wa Mbali
- Heri Kuwa Kibichi Kuliko Kuungua
- Hesabu Ni Kina Cha Werevu
- Ibada Ina Nguvu Kuliko Silaha
- Imani Ya Mitume Haina Kinyume
- Inda Ya Mbwa Kumzuia Ngo’mbe Kula Nyasi
- Jahazi Likipasuka Kila Abiria Ashike Ubao Wake
- Jambo La Ukucha Halichukuliwi Shoka
- Jaribu Huleta Dhahabu Na Matulubu
- Jikune Ufikiapo,Usipo Fikia Paache
- Jina La Sifa Huletwa Na Matendo
- Jina La Mzaha Sawa Na Jeraha
- Jogoo Halali Na Kichwa Chake Shingoni
- Johari Ya Mtu Ni Mbili , Akili Na Haya
- Juhudi Si Kupata , Kupata Majaliwa
- Kalamu Haifutiki ,Neno Husahaulika
- Kazi Ya Usiku Haitoi Jasho
- Kazi Ya Ukweni Huvunja Kifua
- Kazi Ya Siku Moja Haijengi Mji
- Kiburi Ni Vazi Bora Kwa Mungu, Baya Kwa Mlimwengu
- Kifua Chake Nyumba Ya Udongo Haki Himili Vishindo
- Kila Mlango Una Komeo Lake
- Kila Mnyamavu Ni Mwerevu
- Kila Mshupavu Ni Mpumbavu
- Kila Sifa Huleta Maafa
- Kilema Cha Kutafuta Hakipewi Pole
- Kina Cha Bahari Hupimika,Uketo Wa Moyo Wa Mtu Haupimiki
- Kipya kinyemi ingawa kidonda
- Kiranga cha kutafuta hakina majuto
- Kisahafu hakiishi uchafu
- Kivuli cha mti adhuhuri hufunika shina lake
- Kiwi bora kuwa nacho kuliko kukosa kamwe
- Kosa ni utelezi huangusha chini kila rika
- Kua kama mgomba ,mnazi hukawia METHALI ZA KIUTANDAWAZI John P. Mbonde Utangulizi Katika kuziainisha methali, watu hupenda kuziita kuwa hizi ni za asili ya jamii fulani kama vile ya Kihispania na zile ni za Kiafrika au hizi ni za Kimaasai na hizo ni za Kingoni n.k. Aina hii ya methali, jamii huzidai kuwa ni za asili ya jamii yake (kabila fulani), na hivyo, huzifanya kuwa ni mali yake kiutamaduni kama zilivyo mila na desturi tofauti mbalimbali katika jamii hiyo husika. Kumbe kati ya methali hizo zote, baadhi yake hutumika mahali pote duniani. Aina hii ya methali zitumikazo mahali pengi duniani, ingawa huundwa katika lugha tofauti mbalimbali na wakati mwingine kwa mipangilio yake ya maneno hutofautiana, lakini maana yake huwa ni ileile. Ni kwa mantiki hiyo, nimeamua kuziita Methali za Kiutandawazi. Nafahamu pia kwamba baadhi ya wanataaluma wangependa kuziita ni Methali za Kimataifa. Jina lolote linaloweza kutumika kuainisha methali hizo, halina utata wala mjadala kwa kuwa zinatumika miongoni mwa mataifa mengi duniani kote. Kamwe methali hizo siyo mpya wala za ajabu wala hazina hadhi ya milenia ya tatu kwa maumbile, bali ni zilezile ambazo zimezoeleka katika matumizi ya kila siku. Ila inawezekana kwamba zinaweza kuwa za asili ya jamii fulani zilizoanza kuzitumia, au hupendelea kuzitumia mara nyingi zaidi kuliko jamii nyingine kwa msukumo wa mazingira. Kwa mfano, lugha ya Kispanishi ina utajiri mkubwa sana wa methali kuliko lugha nyingi duniani. Hali kadhalika, Kichina kimefaulu kuhifadhi methali zake kwa wingi tangu karne na karne. Madhumuni ya kuzikusanya na kuzihifadhi pamoja ni kurahisisha upatikanaji wake. Fauko ya hayo, huu ni wakati muafaka wa kuzijengea uhalali na hadhi yakinifu methali za kiutandawazi ili kwenda sambamba na maendeleo endelevu ya kisayansi na kiteknolojia. Ifahamike wazi kuwa bado suala hilo linahitaji kufanyiwa tafiti za kina kirefu ili kuboresha dhana hiyo. Mwenendo wa methali za kiutandawazi hautofautiani na ule wa methali za kawaida. Ni dhahiri kuwa baadhi ya vigezo vya kubainisha methali za kiutandawazi ni ile tabia ya taswira za kimataifa zilizobebwa nazo. Baadhi ya methali huhusishwa na vitu vya eneo dogo la nchi, lakini zile za kiutandawazi hazina mipaka. Kwa mfano, Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba. Pemba ni kisiwa katika bahari ya Hindi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilemba ni vitambaa wafungazo vichwani. Tabia ya kufunga vilemba vya aina hiyo, hujitokeza huko Pemba miongoni mwa Waarabu katika mashamba ya karafuu. Ingawa maana ya ndani ya methali hii yaweza kabisa kuwa ya kimataifa, yaani ya kiutandawazi. Mathalani, wazungu watawapendelea wazungu wenzao. Ufinyu wa methali za mahali ni sawa na jinsi aina fulani za mila hutawala jamii ndogo ya mahali hapo tu. Kumbe methali Wapiganapo tembo, nyasi huumia (When elephants fight, the reeds get hurt), hii ni methali ya kiutandawazi. Kwa upande mwingine, baadhi ya methali huwa hazitumiki kila siku, katika ufinyu au utandawazi wake, badala yake huwa zimebaki katika vitabu tu. Ukweli ni kwamba hata baadhi ya misamiati katika kamusi za aina zote za lugha, hubaki katika vitabu kwani matumizi yake ni ya nadra mno kwa sababu au bila sababu za kimsingi. Na kila zinapotumika husikika kuwa ni ngeni katika masikio ya wasikilizaji wake. Hata nchini Tanzania ambako ni chimbuko la historia ya Kiswahili, hususan Zanzibar, kwa namna moja au nyingine, Waswahili hao, si hoja kama ni wasomi au watu wa kawaida, wanaposikia mtu akitumia msamiati au istilahi iwayo utawasikia wakishutumu, "Kiswahili cha siku hizi ni kigumu, jamani! Afadhali ya Kiingereza." Vivyo hivyo, iwapo Mwiingereza msomi akitumia misamiati isiyotumika katika maisha ya kila siku ya jamii ya Waingereza, wanaposikia hayo hulaani na kusema, "Kiingereza cha wasomi wa siku hizi ni kigumu (bombastic). 1.0 Nini maana ya methali? Methali ni lugha nyepesi ipenyayo moja kwa moja katika mioyo ya wasikilizaji. Aidha, methali au misemo huondoa wingu au ukungu katika mawasiliano ya kisayansi na ya teknolojia nzito za kitaaluma. Pia, methali ni kielelezo cha utashi wa uhai wa jamii husika, historia na falsafa ya utu wa binadamu, hekima na busara. Mwanafasihi mashuhuri katika Afrika, Chinua Achebe, katika kitabu chake Things Fall Apart (1959: 7) anaandika, "Methali ni mafuta ya mawese ambayo kwayo maneno huliwa." Kauli hii ikizingatiwa barabara huyafanya maandishi kukubalika kuwa ni fasihi, maana matumizi ya methali na fani nyingine hukoleza simulizi kama tui la nazi na viungo mbalimbali kama vile vitunguu, nyanya, zinavyoifanya mboga iwe na riha na ladha tamu zaidi. Methali ni njia ya mkato ya kuelimisha, kuadilisha, kukosoa na kuelekeza jamii, husuan vijana katika kuzingatia tunu za jadi kwa kina ndani ya mazingira ya asili ya jamii. "Methali ni aina ya usemi nzito na ambao unakusudiwa kusema jambo maalumu lakini ya fumbo. Usemi huu mzito mara nyingi hukusudiwa kumuonya, kumuongoza, na kumuadilisha mwanadamu. Kwa umbile la nje methali huwa na muundo maalumu, muundo wenye baadhi (pande) mbili. Upande mmoja wa methali huwa unaeleza mazoea au tabia ya mtu au kitu juu ya utendaji wa jambo; na upande wa pili unaeleza matokeo yatokanayo na mazoea hayo au tabia hiyo ambayo imeelezwa katika upande wa kwanza." (S. Y. A. Ngole na Lucas N. Honero, Fasihi- Simulizi Methali: Kitabu cha pili, (uk viii) TUKI, DUP 1981. Lugha ya Kiswahili ni tajiri sana kwa semi zake. Licha ya methali, kuna misemo, misimu, nahau. Tofauti na methali misemo ni tungo zitumiazo picha, ishara na tamathali kueleza kitu au wazo kwa kifupi, ili litolewe maadili au maonyo au sifa fulani. Kumbe vitendawili ni semi fupifupi za fumbo zenye kutumia picha, tamathali na ishara kueleza wazo lililofichika ambalo ndilo jawabu la fumbo. Kwa mfano, Koti la mzee halikosi chawa. Na kwa upande wa misimu ni semi ndogondogo za kuibuka na kufifia au kufa kabisa ambazo huzushwa katika mazingira fulani, hufa baada ya mazingira yale kutoweka. Kwa mfano, Klabu ya Simba ilishinda kwa kishindo cha tsunami.(This coinage was heard by the author while travelling in Dar es Salaam comuters known as "Daladala" hence I personally call such sayings as "Daladala Philosophy" which associate with contemporary events such as ‘tsunami’ impact in which Simba soccer club beat their long time rival, the Younger soccer club with such impact as that of tsunami). Pia, matumizi ya msimu, k.m. Mambo! Poa! Huu ni msimu uliochipua na kuchanua miaka hii ya karibuni, ambao nao siku itafika utanyauka na kufa. Hata Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ameondokea kuupenda na kuutumia mara nyingi sana anaposalimiana na wananchi kabla ya kuzungumza au kuwahutubia. Akisha sema, "Mambo!" Hadhira humkubalia kwa mkupuo mmoja, "Poa!" "Methali hutupa maarifa; hutupa ukweli kwa kifupi; hufanana katika lugha mbalimbali za nchi kadha za ulimwenguni; hutumika hasa na wazee kufundisha vijana na watoto, hali ya maisha duniani." Kutoka katika Utangulizi wa kitabu 500 Haya Proverbs kilichotungwa na Nestor, H. Byera, EALB (1978). Aidha, kuna ufafanuzi wa aina mbalimbali kutoka kwa wanataaluma wa nyakati mbalimbali kuhusu dhana "methali". Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu 1981: 165 "Methali ni kifungu cha maneno yanayotumiwa pamoja kisanii kwa njia ya kufumba au kupigia mfano na ambacho kinachukua maana ndefu na pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa; muhtasari wa maneno ya kisanii wenye maana pana k.v. Mcheza kwao hutunzwa." Kuna baadhi ya hadithi nyingi huanza na methali na kumalizia kwa methali. Kwa mfano, katika kitabu kilichotungwa na Kayombo, Innocent Kapilima, Hadithi za Babu Zetu wa Tanganyika, TMP (1959), ametumia mtindo huo wa kuanza na ‘methali’ na kumalizia na methali katika kusimulia hadithi zake. Zipo methali nyingi ni za Kiafrika pale zinapohusisha na ishara au vitu vipatikanazo katika mazingira yao. K.m. "Jifya moja haliinjiki chungu." 2.0 Nini Maana ya Utandawazi? Dhana ya utandawazi ilizuka mwishoni mwa miaka ya 1980 na kushamiri miaka ya 1990 na kuwa changamoto katika nyanja mbalimbali. Utandawazi ni upanukaji kwa kina kirefu zaidi na kusambaa kwa masafa marefu mahusiano miongoni mwa jamii mbalimbali mintarafu uhalisia wa maisha, kuanzia yale ya ustawi wa jamii hadi yale ya harakati za kujikimu, kiuchumi, kiutamaduni, kiulinzi, kibiashara, kiuwekezaji, kimawasiliano, kiteknolojia na kuufanya mchakato mzima kuipelekea dunia iwe mithili ya kijiji kimoja kidogo. Mvuvumko huo wa kiutandawazi kiuchumi na kiutamaduni umeipa Marerkani nafasi ya kasi kubwa ya katika kuhodhi na kudhibiti mageuzi hayo. "Kwa ufafanuzi wa jumla, dhana utandawazi inamaanisha kuifanya dunia nzima ionekane kama kijiji kimoja kwa kupanuka kwake kimawasiliano, kijamii na kiuchumi katika uhalisia wa mambo ulivyo katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, utamaduni, biashara, uwekezaji, kiteknolojia hata kiroho. Kutokana na welewa huu inadaiwa kwamba uchumi wa dunia umo katika mchakato wa kuoanishwa kwa kuvunja mipaka na nguvu za kiuendeshaji kuwa kitu kimoja." S.M.Rugumamu, Globalization Demystified, DUP (2005). Waandishi wengine, kama vile C.K. Omari, Prof. E. Kezilahabi na W.D. Kamera wanasisitiza katika vitabu vyao Misemo na MethaliToka Tanzania (Kitabu cha I&II): "Misemo na Methali zimejaa wingi wa hekima na mafundisho yanayoweza kutumika katika kufafanua utamaduni wa jamii, muundo na mfumo wake, siasa yake, uchumi na mazingira yake." 3.0 Mantiki ya Methali za Kiutandawazi Nimeorodhesha baadhi tu ya methali zenye hadhi ya utandawazi na kuelezea kwa kifupi kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, ingawa ingependeza sana kama tafsiri yake ingeweza kuwa katika lugha ya Kifaransa, Kijerumani, Kichina na katika lugha zingine za kimataifa. Ukweli huu wa methali za kiutandawazi unaenda sambamba kama alivyoandika Hellen Byera Nestor katika utangulizi: "…methali hufanana katika lugha mbalimbali za nchi kadha za ulimwenguni." Hapa mwandishi huyo kwa kutumia dhana ‘hufanana’ kimsingi alimaanishwa kuwa baadhi ya methali hutumika mahali pengi duniani ingawa ni kwa lugha tofauti lakini maana iliyobebwa katika maudhui yake ni ileile. Zimepangwa kwa kuzingatia alfabeti ya Kiswahili. Methali za kiutandawazi ni changamoto kwa upande wa maendeleo ya mawasiliano ya kiuhusiano miongoni mwa mataifa. Ikumbukwe kwamba madai kwamba methali za kiutandawazi asili yake ni Ulaya au Marekani kama inavyodaiwa katika masuala mengine mengi ya kiutamaduni na kihistoria. Utajiri uliomo katika methali za kiutandawazi kamwe usimithilishwe na utajiri au maendeleo mengine ya kisayansi na kiteknolojia kutoka katika nchi tajiri duniani na kwenda nchi maskini duniani! Ni matumaini yangu kwamba mkusanyiko huu wa methali za kiutandawazi utatoa changamoto kwa wanataaluma kujenga wigo mpana na kukita katika kina kirefu cha uchambuzi na upembuzi yakinifu. 4.0 Changamoto Watu binafsi, serikali na taasisi mbalimbali zinaendelea kupania katika kukikuza Kiswahili. Kutokana na hali halisi ya baadhi ya methali kuweza kupotea miongoni mwa jamii mbalimbali za Kiafrika, mpango maalumu umeanzishwa ili kuweza kuziandika na kuzitolea maelezo methali za makabila mbalimbali ya Afrika kwa kuandika vitabu kadha wa kadha. Mradi huo ambao kila mwezi hutoa methali moja kutoka nchi moja ya Kiafrika, unaweza kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and Stories Website: www.afriprov.org. Hali kadhalika, kuna vitabu vingi vya methali vilivyoandikwa na watunzi mbalimbali duniani. Katika mradi nilioutaja hapo juu, jitihada zimefanywa na kila mwandishi katika kukumekusanya methali zisizopungua mia moja za jamii yake kwa shabaha ya kuzihifadhi ili zisije zikapotea. Mradi wa methali adimu za Kiafrika ulioanza mwaka 1999 ilimradi kusalimisha methali na misemo ambayo iko hatarini kupotea, hadi 2004 ulikuwa umefaulu kuzikusanya na kurudufu vijitabu kumi na tatu. Kuna tegemeo kubwa kupata ongezeko kubwa kabla ya mwisho wa mwaka huu 2005. 5.0 Hitimisho Tunaposherehekea Jubilei ya Miaka Sabini na Tano (75) ya mchakato wa kukistawisha Kiswahili (The Inter-Territorial Language [Swahili] Committee iliyoundwa 1930 hadi Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI), iliyopandishwa hadhi mwaka 1964), bado safari ni ndefu. Juhudi mbalimbali zilifanywa na serikali hata ikaunda Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) 1967; Idara ya Kiswahili-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1970; Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni, Zanzibar 1979. Na wakereketwa waasisi walianzisha Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) tangu miaka mingi kabla ya kupata Uhuru mwaka wa Tanganyika. Kiswahili hutumika katika nchi nyingi duniani; hufundishwa katika taasisi na vyuo vikuu kadha wa kadha duniani; hutumika katika vituo vya redio na televisheni nyingi duniani; aidha, ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika (AU). Zifuatazo ni baadhi tu ya methali za kiutandawazi: METHALI ZA KIUTANDAWAZI 1. Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo Kutokana na tabia ya kibinadamu, mtu hutambulika kwa uungwana wake kwa vitendo vyake wala siyo kwa mavazi, maumbile au maneno ayasemayo. Public opinion maintains, a gentleman is judged by his actions. (Manners make man; or Handsome is as handsome does). 2. Akili ni nywele kila mtu ana zake Akili za watu ni za aina nyingi na ni tofauti kama vile nywele za kila binadamu ni tofauti. Brains are like hair, every humankind has her/his own kind. 3. Baada ya dhiki faraja Baada ya shida huja raha. After hardship comes relief. (Every cloud has a silver lining; After storm comes a calm). 4. Bandubandu huisha (humaliza) gogo Hata gogo liwe kubwa namna gain, unapolichanachana mwisho gogo hilo humalizika. Chip! Chip! Finishes the log. (Little strikes fell great oak. Constant dripping wears away a stone). 5. Chanda chema hufikwa (huvishwa) pete Jambo jema husifiwa na hushangiliwa ili liweze kufana zaidi. Ni wana kama kidole kizuri kinapovalishwa pete ili kizidi kupendeza. A handsome finger gets a ring put round it. 6. Chema chajiuza kibaya chajitembeza Kitu kizuri huonekana bila ya kunadiwa, lakini kibaya hupigiwa debe ili kukitangaza. A good thing sells itself, a bad thing advertises itself for sale. (Good wine needs no bush). 7. Dalili ya mvua ni mawingu Ishara ya kuwa mvua itanyesha hivi punde ni mawingu meusi makubwa. Na yasipokuwepo mawingu haiwezi kunyesha. Hali kadhalika, katika juhudi zako waweza kujua mapema kama utafanikiwa. Clouds are the sign of rain. (Morning shows the day as the childhood shows the man. Cunning events cast their shadows before. No smoke without fire). 8. Damu ni nzito kuliko maji Watu wa ukoo mmoja husaidiana sana katika matatizo yao kuliko marafiki au jamaa wa mbali. Blood is thicker than water. 9. Elimu haina mwisho Elimu ni za aina nyingi. Kila siku maarifa ya aina mpya yanagunduliwa na kuzuka, hivyo haiwezekani kuielewa elimu yote duniani. Education has no limits. (One has to continue to learn all his/her life time). 10. Elimu ni bahari Elimu ni pana hivi sawa na upeo wa bahari ambayo huelezwa na kusambazwa miongoni mwa binadamu. Education is like an ocean which spread all over the horizons of people’s life. 11. Fadhili za punda ni mashuzi Shukrani za mtu mjinga ni kumtukana yule aliyemtendea mema. The gratitude of a donkey is a breaking of wind. 12. Fimbo ya mbali haiuwi nyoka Fimbo iliyo karibu nawe ndiyo ikufaayo wakati inapotokea shida. Methali hii inalenga kuwatanabaisha watu kuwa binadamu anapopata shida ni watu walio karibu naye ndio watakaomsaidia. A stick in the hand is the one that kills a snake. 13. Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno Ganda la jana la muwa huwa limekauka, lakini chungu anapolipata huona ni mavuno maridhawa. Maana asiyezoea kuwa nacho, akipatapo hata kama ni kitu duni au hafifu namna gani na kidogo, hushangilia. Mathalani, kukengeuka kwa maadili kwa vijana barani Afrika na kuzamia tamaduni za kigeni. The skin of yesterday’s sugar-cane is a whole harvest of an ant. 14. Gonga gogo usikie mlio wake Ukitaka kujua mlio wa gogo, lipige na usikilize. Hili lina maana kuwa yakupasa kulichunguza jambo kwanza kabla ya kulihukumu (kulikabili). Knock a log in order to hear the sound it makes. 15. Haba na haba hujaza kibaba Ukiweka akiba kidogo ya kitu kila mara, mwishoni utakuwa na akiba kubwa. Mwanzo wa makubwa ni madogo. Little by little fills up the measure. (Little drops of water, little grains of sand, make a mighty ocean and a pleasant land). 16. Harakaharaka haina baraka Jambo lifanywalo harakaharaka, haliwezi kufana. Mambo lazima yaende kwa kuzingatia mchakato wenye mpango na taratibu madhubuti. Hurry, hurry, has no blessing. (More haste, less speed). 17. Iliyopita si ndwele, ganga ijayo Mambo yaliyopita, yasishughulikiwe sana, bali tujizatiti kuyakabili na kuyadhibiti yale yajayo. That which has passed is not a diease, cure what is coming. 18. Iwapo nia, njia hupatikana Mtu anapofanya dhamira ya dhati ya kutaka kulitekeleza jambo, hawezi kukosa njia ya utekelezaji. Where there’s a will, there’s a way. 19. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza Chochote usichokifahamu vizuri huwezi kukieleza kwa ufasaha. A matter of which you are ignorant is like a dark night. 20. Jogoo la shamba haliwiki mjini Jogoo lililozoea kuishi shamba, likihamishiwa mjini hushindwa kuwika kwa sababu ya mabadiliko ya mazingira yake. Maana, ye yote aliye ugenini yampasa kufanya mambo kwa tahadhari ili kulingana na mazingira ya hapo. The country cock does not crow in the town. 21. Kata pua uunge wajihi Mtu akikata pua yake kwa ajili ya kujirembesha anakuwa anaiharibu sura yake zaidi. Cut off your nose to mend your face. (Keep up appearances even at the price of losing your property. Cut off your nose to spite your face). 22. Kidole kimoja hakivunji chawa Mtu mmoja peke yake hawezi kutenda mengi. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. One finger cannot kill a louse. 23. Kuishi kwingi kuona mengi Kuishi katika dunia kwa muda mrefu humpa mtu nafasi ya kujifunza mengi. Tuwaheshimu wazee kwa vile wanaweza kutushirikisha katika mang’amuzi mengi yenye hekima na busara. To live long is to see much. 24. La kuvunda halina ubani Harufu mbaya ya kitu kilichooza haiwezi kufichika au kuzuiwa kwa kufukizia ubani. Hali kadhalika, jambo lililoharibika halifichiki. There is no incense for something rotting (it is impossible to conceal its evil odour). 25. Lililoandikwa ndilo liwalo Lile aliloliweka Mungu litendeke, halishindwi kutendeka kama alivyolipanga. Hii ina maana kuwa Mwenyezi Mungu ni muweza wa yote, hivyo alipendalo hutokea vivyo hivyo. Hakuna awezaye kushindana na matakwa (mapenzi) ya Muumba. That which is written (by God) is what is (i.e. must surely come to pass). 26. Maji yaliyomwagika hayazoleki Maji yakisha mwagika haiwezekani kuyazoa au kuyakusanya tena. Yaani, jambo likiharibika huwa limeharibika, hata kama likitengenezwa kamwe halitaweza kuwa kama lilivyokuwa hapo awali. If water is spilt, it cannot be gathered up. 27. Milima haikutani, lakini binadamu hukutana Milima haina uwezo wa kukutana, lakini binadamu wakiwa hai huweza kukutana hata baada ya kuwa mbalimbali kwa muda mrefu. Hii ni methali inayotumika katika kutiana moyo wakati wanapoagana kwamba wakijaliwa watakutana. Pia hutumika katika kuwaonya watu kuacha tabia ya kuwatendea vibaya wengine kwani huenda wao pia wakatendewa hivyo siku za usoni. Mountains do not meet, but people meet each other. 28. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo Malezi umpatiayo mtoto huwa ni msingi wa mustakabali wake. Maisha ya mtu yanategemea sana msingi wa malezi aliyoyapata tangu angali mchanga. Ni vigumu kwa mtu kuacha tabia aliyoizoea katika makuzi yake. As you bring up the child, so he/she will be. 29. Njia mbili zilimshinda fisi Kutokana na tamaa yake kubwa, fisi alijaribu njia mbili ya kushoto na kulia, lakini alishindwa. Mwangata mbili, moja humpokonya. Two ways failed the hyena. 30. Nyumba usiyolala ndani yake hujui ila zake Mtu hufahamu tu mambo ya nyumba ambamo amelala. Ni jambo la kijinga kwa mtu kujifanya kuwa anaelewa mambo ambayo kwa yamkini hayaelewi. You cannot know the defects of a house you have not slept in. It is the wearer who knows where the shoe pinches. 31. Ombaomba huleta unyonge Tabia ya kuombaomba vitu humfanya mwombaji kuwa mnyonge au duni. Mlegevu, mzembe, goigoi na mvivu kuwategemea watu wengine, maana hana bidii ya kujitafutia riziki yake kwa kufanya kazi mwenyewe. Mtegemea cha ndugu, hufa maskini. Begging makes somebody become inferior. 32. Ondoa dari uezeke paa Acha kujenga dari mpaka umalize kuezeka. Mtu anatakiwa kwanza kufanya jambo lililo muhimu kwanza kabla ya mengine yasiyo muhimu. Remove the ceiling in order to thatch the roof. 33. Panapofuka moshi pana moto Moshi ni ishara ionyeshayo uwepo wa moto. Watu wanaogombana mara kwa mara si ajabu kuwa siku moja wataingia vitani na kusababisha maafa. Where there is smoke there is fire. 34. Paka akiondoka, panya hutawala Paka na panya ni maadui wakubwa. Paka hutishia sana uhai wa panya kwa kuwakamata na kuwala nyama. Kwa jinsi hiyo, paka anapoondoka, panya hupata nafasi ya kufanya vitu vyao bila ya kuwa na hofu yoyote. Ndivyo ilivyo kwa wafanyakazi, endapo mkubwa wao akiondoka, walio chini hujiona kuwa huru na hufanya mambo wapendavyo. When the cat goes away, mice do reign. When the cat’s away, the mice do play. 35. Penye watu wengi hapaharibiki neno Mahali ambapo kuna watu wengi hapaharibiki neno. Walipo watu wengi hubadilishana mang’amuzi na hivyo fikira na nguvu zao hukusanywa pamoja ili kulitengeneza jambo. Penye wengi pana Mungu ambaye ni muweza wa yote. Where there is a gathering of people nothing goes bad. Where there are many people, there God is (Vox populi vox Dei). 36. Radhi ni bora kuliko mali Kupata radhi ya wazazi ni bora kuliko kupata mali. Baraka ya wazazi haiwezi kupatikana hivihivi tu, lakini mtu anaweza kutafuta mali wakati na mahali popote. Kwa hiyo, yatupasa kuwatii wazazi (wakubwa) wetu ili watubariki ndipo hata tutafutapo mali au riziki huwa tumekwisha pata baraka ya mafanikio maishani kutoka kwa wazazi. Blessings are better than wealth. 37. Rahisi haihalisi Kitu au bidhaa ipatikanayo kwa bei poa ni kitu hafifu hivyo huwa si kizuri na hakifai. Cheap things are not worthy spending money on them. 38. Sikio halilali njaa Hapana siku ipitayo bila ya sikio kusikia maneno fulanifulani yawe mabaya au mazuri. Hivyo sikio halilali bila ya kusikia neno. An ear does not go to sleep hungry (there’s always plenty of gossip). 39. Sumu ya neno ni neno Moto huzimwa kwa maji na pia neno humalizwa na neno. Likizuka neno au jambo linalowafanya watu kulisema sana au uvumi fulani, ule uvumi huendelea hadi pale uvumi mwingine tofauti utakapotokea. Basi, hapo watu husahau ule uvumi wa kwanza wakaushika ule uvumi mpya. The poison for a word is a word. Tit for tat. 40. Tamaa mbele, mauti nyuma Mtu mwenye tamaa nyingi mwishowe hupatwa na misiba mibaya. Anayetanguliza tamaa na ubinafsi mbele ajue hana mwisho mzuri. Desire first, death afterwards (i.e. No one ever thinks of the possibility of death when concentrating on achieving a particular end). Man proposes, God disposes. 41. Taratibu ndio mwendo Mwendo wa polepole ndio ufaao. Yaani, jambo lolote lile halina budi kufanywa kwa kuzingatia kanuni. Slowly is indeed the way to walk. He that goes slowly goes surely. Hasten slowly. Slow but sure. 42. Uchungu wa mwana, aujua mzazi Mzazi ndiye anayepata uchungu mwingi zaidi ya watu wote anapomzaa mtoto wake. Yaani mwenye kuthamini kitu chochote kile ni yule mwenye kitu hicho. Kwani ni yeye ndiye aliyetaabika katika kukitafuta na kukipata. The labour of childbirth is known to the mother. 43. Ukiona vinaelea, vimeundwa Ukiviona vyombo vya kusafiria vinaelea juu ya maji, ujue kwamba ni matokeo ya juhudi na maarifa ya watu waliovitengeneza. Kizuri chochote ukionacho, ufahamu kimepatikana kwa bidii na jasho na siyo kwa miujiza. If you see vessels afloat, remember that they have had to be built. 44. Usipoziba ufa, utajenga ukuta Usipoukarabati ufa kwenye ukuta mapema, ukuta utabomoka na hivyo utalazimika kuujenga ukuta tena. Usipolirekebisha kosa dogo tangu mwanzo, utapata hasara kubwa hatimaye. If you do not fill up a crack, you will have to build a wall. A stitch in time saves nine. 45. Vita havina macho Wakati wa vita mtu ye yote yule anaweza kuumizwa, kuuawa au kupata madhara ya aina yoyote ile. Ni vema kujiepusha na vita. War has no eyes (i.e. it kills indiscriminately). 46. Vita vya panzi furaha ya kunguru Panzi wanapopigana na kuuana kwa wingi ni furaha ya kunguru kwani hupata chakula chao kwa urahisi. Hali kadhalika, maafa ya wanyonge huweza kuwa furaha ya wakubwa. A fight between grasshoppers is a joy to crows. 47. Wapiganapo tembo, nyasi huumia Ndovu wawili wakipigana, husababisha nyasi kukanyagwakanyagwa na kuharibika. Yaani viongozi wawili wanapopigana wanaoumia ni wafuasi au watu walio chini ya himaya zao. Wakati mataifa makuu mawili (k.m.Warusi na Marekani wakati wa vita baridi) yanapopigana, mataifa madogo ndiyo yanayoumia. Where elephants fight, the reeds get hurt. 48. Ya kale hayapo Yale yaliyotokea zamani yamekwisha na yanapaswa kusahauliwa. Hapana haja ya mtu kuwa na kifundo cha moyo kwa ubaya aliofanyiwa hapo zamani. The ancient (things) are no longer with us. Let bygones be bygones. 49. Yote yang’aayo si dhahabu Si kila kionekanavyo kinameremeta ni dhahabu. Kwani viko vingi ving’aavyo, lakini ambavyo si dhahabu na ni vya thamani ndogo mno kuliko dhahabu. Usikipende kitu kwa uzuri wake wa nje, bali ukichunguze sana ili ujue ubora wake. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti. All that glitters, do not think it is gold. 50. Ziba mwanya, asipite panya Ukisha kugundua mwanya wa panya, fanya hima ili uuzibe ili panya wasifanye mazoea ya kuutumia mwanya huo. Mathalani, serikali ikisha gundua mwanya wa bidhaa za magendo haina budi kuharakisha kuuziba mwanya ili kuondokana na ugumu wa kulikabili tatizo hilo baada ya kuzoeleka na walanguzi seuze na wafanyabiashara ya magendo. Seal the small path so that the rats should not create the habit of using it. 51. Zimwi likujualo halikuli likakwisha Shetani akujuaye hakuli akakumaliza. Watu wa jamii au ukoo moja hawadhuriani kabisa. Endapo wakifanya hivyo, basi huhesabika kuwa ni wachawi. A devil that knows you will not devour you completely. Vitabu vya Rejea 1. Ahmed Ndalu & Kitula G. King’ei, Kamusi ya Methali za Kiswahili, EAEP (1989). 2. Charlotte and Wolf Leslau, African Proverbs, The Peter Pauper Press, NY (1962). 3. Farsi, S.S., Swahili Sayings, EALB 4. Healey, Joseph G., Towards an African Narrative Theology, Paulines Publications Africa (1996); Once Upon a Time in Africa: Stories of Wisdom and Joy, Orbis Books (2004); African Stories for Preachers and Teachers, Paulines Publications Africa (2005); Kueneza Injili kwa Methali, Benedictine Pulications Peramiho (1984). 5. Johnson, Frederick, Swahili-English Dictionary & English-Swahili Dictionary, OUP (1939). 6. Kalugila, Omushumba Leonidas, Emigani na Ebikoikyo, North Western Publishers, Bukoba (1992). 7. Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, Kugundua Mbegu za Injili, Benedictine Peramiho Publications (1993). 8. Madam, Swahili-English Dictionary, (1894). 9. Mayoka, J.M., Nahau za Kiswahili, Mathews Bookstore & Stationers, Dar es Salaam, Tanzania. 10. Mbonde, J. P., Wisdom from Ngoni Proverbs, privately duplicated (2004). 11. Muwanga, Aminieli Stephano, Methali kwa Picha, Utamaduni Publishers (1984). 12. Ngole S.Y.A. & Honero Lucas N. (Wahariri), Fasihi Simulizi Methali (kitabu cha Pili (TUKI) DUP (1981). 13. Nestor, Hellen Byera, 500 Haya Proverbs, East Africa Literature Bureau (1978). 14. Omari,C.K., Kezilahabi, E., and Kamera,W. D., Misemo na Methali Toka Tanzania Kitabu cha 1 (Toleo Jipya 2000) & Kitabu cha 2 (Toleo Jipya 2004) Mathews Bookstore & Stationers, Dar es Salaam, Tanzania. 15. Rugumamu, Severine M., Globalization Demystified: Africa’s Possible Development Futures, DUP (2005). 16. Scandinavian Institute of African Studies: Swahili Proverbs from East Africa, Uppsala (1977). 17. TUKI: Kamusi ya Kiswahili Sanifu, OUP (1981). 18. TUKI: Kiswahili cha Utandawazi, DUP 19. TUKI: Kamusi ya Kiswahili Sanifu (toleo la pili), OUP (2004). 20. Wamitila, K.W., Kamusi ya Methali, Longhorn Publishers, (2001). 21. Wanjohi, Gerald Joseph, Under One Roof- The Gikuyu Proverbs; & The Wisdom and Philosophy of African Proverbs: The Gikuyu World-View, Paulines Publications Africa (1997) Note: This paper was originally delivered during the 75th anniversary of TUKI or the Institute of Kiswahili Research (1930-2005) at the University of Dar as Salaam, Tanzania (4th-7th July, 2005). The author decided to select only 51 proverbs that are commonly used around the globe. Hence, he calls them "global proverbs." Actually, globalisation as a process commenced many centuries ago. Think of the early travellers such as Christopher Columbus, Vasco da Gamma, missionaries, slavery and slave trade, the First and Second World Wars and other periods and other events. One evidence is Negro-Americanism with its complexity of cultures. But globalisation takes a new face in the development of economy and culture particularly science and technology in communication. The third millennium appears to have overshadowed the entire meaning of globalisation. The contextulisation of each global proverb varies according to its environment and culture. But those of African origin have their flavor or touch notched in each one of them: e.g. Proverbs are the daughters of experience (Sierra Leone); A proverb is the horse of conversation: when the conversation lags, a proverb will revive it (Yoruba); A wise man who knows proverbs reconciles difficulties (Yoruba). Indeed, these few selected global proverbs in this paper are intended to represent all those that which
151 Mshale hurudi kwao ukipotea porini
152 Mtaratibu humshinda mwenye nguvu
153 Mtego bila chambo haunasi
154 Mti hauendi ila kwa nyenzo
155 Mti huponzwa na matunda yake
156 Mti ulio ukweaa ni rahisi kuu shuka
157 Mtindi hau haribu shoka
158 Mtoto akinyang’anywa kisu hupewa banzi aka chezea
159 Mtoto anakazi arubaini kwa siku
160 Mtoto akiomba samaki hapewi nyoka
161 Mauti hutembea na mganga
162 Mtambua ndwele ndie mganga
163 Mwalimu alivyo ndivyo mwanafunzi huwa hivyo
164 Mwanamke hupenda aliye machoni pake,akiondoka analake
165 Mwana wa kuku hafundishwi kuchakura
166 Mweka mwiku hula na wenziwe
167 Mwenda omo na tenzi hurejea ngamani
168 Mwenye subira hajuti
169 Mwivi hushikwa na mwivi
170 Mwungwana hanuni mashavuni hununa moyoni
171 Mzigo usio uchukua hujui uzito wake
172 Mzoea koka hali cha kupika, akila hutapika
173 Mzoea twaa,kutoa ni vita
174 Ndoa mbaya afadhali kuliko ,ujane mwema
175 Ndondo si mlisho[haizamishi chombo]
176 Ng’ombe akivunjika mguu malishoni, hurudi zizini
177 Ng’ombe mwenye mkia,akikimbia huvuta wengine kumfuata
178 Ng’ombe mtangulizi hanywi maji machafu
179 Ngozi ya paa hawakai watu wawili
180 Nisikose kaa na gando
181 Njaa humfuga samba
182 Nyani haoni mando lake
183 Nyumba hutegemea miti kama nchi kwa mabinti
184 Nyumba ni mwana mke
185 Ombi ukilishika hupati fimbo wala msonyo
186 Ongoa motto njia impasayo
187 Paka wengi hawa shiki panya
188 Pang’opako jino pana pengo
189 Punda alikosa pembe akapewa masikio,alipo lia choyo aliongezewa mlio
190 Pweza kamwambia ngisi,tusifanye majilisi maji ya kipwa, tukisi
191 Raha bila mali karaha
192 Raha bila mali muhali
193 Rahisi kujifunza ,rahisi kusahaulika
194 Rafiki akipenda, anajambo akutenda
195 Samaki akioza ni mtungo pia
196 Sheria pofu lakini inapenda kusikiliza mlio wa fedha
197 Sifa ni chakula cha maiti
198 Sifa ya nguo ni pindo
199 Starehe ya mbwa ni kukalia mkia wake
200 Tabia haifichiki kwa nguo
201 Tamu tulikula wote na chungu vumilia
202 Tumbili akila tamu,hujifanya kala pilipili
203 Ugonjwa suna kufa faradhi
204 Ukija mjini kwa wenye chongo,nawevunja lako jicho
205 UKinyang’anywa chako utakidai kwa lugha ,ukinyang’anywa lungha itakuweje?
206 Ukiona neno usinene neno,ukinena neno litakupata neno.
207 Ukipofuka na utu uzima pawe kwapo chumvi wa pajua
208 Ukipata pembe kula na makame,akiulizwa asikane aungame
209 Ukipooza utapoteza
210 Ukitega nyani ficha kamba kwa majani
211 Ukiwa na watoto acha hasira
212 Ulalaye naye kitanda kimoja, akijikunja hana haja nawe
213 Uta ulio shindia usipouweka uta vunjika
214 Vijiti vingi pamoja vigumu kuvunjika
215 Vimtoshavyo mtu ni sanda na kiunza
216 Waa la tabia hushinda waa la nguo
217 Wafu hawarudi hufuatwa na wazima
218 Watafuta makosa hawaoni kitu kingine ila makosa
219 Wawili hawapotei njia
220 Wema hauna lawama,ubaya una kilema
221 Ya kunyesha haina wingu
222 Yumo katika luja
223 Yalioko unguja na pemba yako
224 Zimwi la kwenu lenu
225 Zohari harabu ya wakati
226 Zani halipendezi kutafuta ila kukutafuta
91. Kuku akiatamia hana matembezi
92 .Kuku wa masikini hatagi ,akitaga haangui, akiangua,wana huliwa na mwewe
93.Kula mbwanda ,si kuwanda
94. Kulia juu, chini kuna moto
95. kwako kuki ungua ,kwa mwenzio kuna teketea
96. kweli msumeno ,mbele unga ,nyuma unga
97. Kweli chungu lakini hupendwa na Mungu
98. Kweli kali lakini halali
99. La kichwa likifika shingoni,halikupotea.
100. Labda ilipo hakika haipo
101. Lako una hiari nalo lenu huna
103. Lifaalo kueleza ,leleza,lisilofaa limeze
104. Lisilo pona huvumiliwa
105. Maagizo matupu haya himizi kazi
106. Maagizo ya mungu hushinda ya mizungu
107. Mbwa mtembezi huokota mifupa
108. Mali huvunja nguu, milima ikalala
109. Mambo yote huhitaji akili ,ila kula
110. Mambo yote haya fai kwa watu wote
111. Masikini hana makuu.
112. Masika si mvua,masika ni kukosa cha jioni.
113 Masikini wa mali yupo, masikini wa jambo hayupo
114. Matendo ya viongozi huwa maongozi
115. Mazao ya fikira ni tendo,mazao ya tendo ni mazoea, mazao ya mazoea ni tabia na mazao ya tabia ni bahati zetu duniani
116. Mazoea huleta dharau
117 Mbegu zikiwa haba huchanganywa na mchanga
118 Mbuzi akichagua nyasi ni mgonjwa
119. Mbwa akiona pwani hafi maji
120. Mbwa umujuaye jina hakuumi
121. Mchaga huahidi akavunja kiaga
122 Mchimba kisima hakatazwi maji
123 Mchimba kisima hakai juu
124. Mchonga mwiko hataki kuungua
125 Mchunga ng’ombe hakatazwi maziwa
126 Mdharau chake ni mwizi
127 Meno ya mbwa haya umani
128 Mfuasi wa fisi hali kitu
129 Mfuasi wa simba hula makombo ya mawindo
130 Mfuasi wa inzi hula uvundo
131 Mfuasi wa nyuki hula asali
132 Mfuasi wa wengine huwa nyuma siku zote,jasirisha uvumbuzi wako mwenyewe
133 Mfufia samba huliwa
134 Mgeni wa usiku hula kitanda
135 Mgonjwa haulizwi dawa
136 Mhisani hufa mwili, hafi jina
137 Mji miwili ina ndoto mbili
138 Mkono uleao mtoto ndio uleao dunia
139 Mjinga akitambua mjanja huwa mashakani
140 Mja haishiwi haja
141 Mla mbuzi hulipa ng’ombe
142 Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa naye
143 Mngereza hutengeneza aka kereza
144 Mlilia nasibu hufa angali masikini
145 Mlinda kisima hakai juu yake
146 Moyo ufikiripo ndiko miguu iendako kila siku
147 Mpenzi hana kinyongo
148 Mrefu halali vitanda viwili
149 Msafiri huonja mapishi mengi
150 Msafiri ni masikini hata kama ni mfalme
Methali za bidii ni gani
ReplyDeleteNice one
ReplyDelete